Burudani

Usher Raymond na mkewe Grace Miguel waachana

Mwaka 2018 umeonekana kuwa ni mbaya kwa wapendanao. Usher Raymond na mkewe Grace Miguel wametangaza kuachana baada ya kupita miaka miwili ya ndoa yao na kudumu kwenye mahusiano kwa miaka 10.

Kwa mujibu wa mtandao wa Us Weekly umetoa taarifa ya wawili hao ya kuachana inayosomeka, “Baada ya kufikiria sana na kuzingatia tumeamua kujitenga kama wanandoa.”

“Tunaendelea kushirikiana kwa ukaribu zaidi, marafiki wa upendo ambao wataendelea kuunga mkono kwa njia nyingine ya maisha yetu. Kiasi kikubwa cha upendo na heshima tuliyo nayo kwa kila mmoja itaongezeka tu tunapoendelea,” imeongeza taarifa hiyo.

Hata hivyo Chanzo cha karibu cha wawili hao kimeuambia mtandao huo, Usher na Grace wametengana tangu miezi michache iliyopita.

Usher na Grace wamekuwa na mahusiano kwa karibu tangu mwkaa 2009 baada ya msanii huyo kuachana na aliyekuwa mke wake, Tameka Foster ambaye walifanikiwa kupata watoto wawili kwenye ndoa yao iliyodumu kwa miaka miwili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents