Burudani
Utafiti: Asilimia 95 ya Watanzania wanataka kuwepo haki ya kuikosoa serikali
Asilimia 95 ya wananchi wa Tanzania wamedai kuwepo na haki ya wananchi kuikosoa serikali.
Wananchi hao ni pamoja na wafuasi wa chama tawala na wale wa upinzani, kwa mujibu wa utafiti mpya wa taasisi ya Twaweza. Matokeo ya utafiti huo uliopewa jina Sauti za Wananchi: Demokrasia, Udikteta & Maandamano, umezinduliwa Alhamis hii jijini Dar es Salaam.
Umebaini kuwa 93% ya wafuasi wa chama tawala wangependa wananchi waruhusiwe kuikosoa serikali inapofanya makosa.
Utafiti huo pia umeonesha kuwa 11% ya wananchi wanaamini kwamba Tanzania inaongozwa na dikteta, huku 58% wakipinga. Pia umedai 29% ya wananchi walio karibu na vyama vya upinzani wanaamini Tanzania inaongozwa na dikteta.