Habari

Utajiri wa Ivanka Trump na mumewe ni hatari

Utajiri wa Ivanka Trump na mumewe Jared Kushner ni hatari. Wawili hao wana mali zenye thamani ya dola milioni 740. Hilo limewekwa wazi na Ikulu ya Marekani kama sheria inavyowataka viongozi wa nchi hiyo kuweka wazi mali zao.

Ivanka aliteuliwa siku chache zilizopita kwenye cheo cha msaidizi wa Rais kama mwajiriwa asiyelipwa mshahara huku mumewe akiteuliwa mapema mwaka huu kuwa mshauri mkuu wa rais. Naye mshauri mkuu wa Trump kuhusu uchumi, Gary Cohn ametajwa kuwa na utajiri wa takribani dola milioni 250.

Inadaiwa kuwa watu waliopo kwenye baraza la mawaziri la Trump wana jumla ya mali zenye thamani ya dola bilioni 12.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents