BurudaniUncategorized

Video: Ally Nipishe ‘achokonoa’ beef la Diamond na Alikiba

Msanii wa Bongo Flava, Ally Nipishe amesema kama ni kweli Diamond na Alikiba wana beef sio kitu kizuri.

Muimbaji huyo amesema katika pande hizi mbili pinzani katika muziki wa Bongo Flava hana upande na zile team zao ni sawa kuwepo endapo zitafanya kazi ya kumsaidia msanii husika.

“Kwanza Diamond Platnumz ni brother yangu, Alikiba ni brother yangu, yaani wale wote ni watu ambao nawaamini sana kwa sababu wao ndio wanasababisa sasa hivi tuone kweli moto upo.

“Kwa upande wangu kuwashauri kaka zangu wale wawili, sijui attention yao ni nini au target lakini kwa kawaida sio poa kwa sababu sisi tunawaangalia wao na beef zile sio sawa,” Ally Nipishe ameiambia Bongo5.

Alipoulizwa kati ya Diamond na Alikiba nani hasa aliyemkosea mwenzake ila aombe msamaha, alijibu, “hapo sijui huwa naona hivyo tu, kwa hiyo sijui nani anamkosea mwenzake hapo, sijawahi kukaa nao ila ni kaka zangu kwenye kazi na pia nawakubalia pia mimi ni sabiki yao, hiyo sijui nani ana makosa”.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents