Burudani

Video: Ben Pol jinsi anavyopokea maoni ya ‘Tatu’

Baada ya Ben Pol kuachia ngoma yake ya ‘Tatu’ wiki chache zilizopita na kuibua maneno mengi kuhusu wimbo huo – mkali huyo wa muziki wa RnB nchini ameendelea kupokea maoni ya wimbo huo ambao wengine wamedai ni mbaya.

Kupitia mtandao wa Instagram, Ben amepost video inayomuonyesha akipitia maoni kuhusu wimbo huo na kuandika, “Unapokuwa unayameza maoni mbalimbali unayopewa kuhusiana na Mwenendo wako (swallowing peoples opinions be like… ).”

Siku kadhaa msanii wa muziki na miliki wa lebo ya Bana Music Records, Baraka The Prince alikaririwa akiongea kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM, wimbo huo ni mbaya. “Nilitegemea Ben Pol angetoa wimbo mkali kutokana na fujo za hivi karibuni alizozifanya muimbaji huyo kwenye mitandao ya kijamii. Ben Pol karisk sana, halafu kaja anatoa nyimbo mbaya. Hapo mimi ndio nilishangaa,” alisema Barakah katika kipindi hicho.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents