Michezo

Mnyama ‘Simba SC’ kuunguruma leo shamba la bibi

Mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (FA), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC), Simba leo watashuka dimbani kumenyana na klabu ya Nakuru All Stars kutoka Kenya kwenye mchezo wake wa kwanza wa Kombe la Michuano ya SportPesa Super Cup.

Tokeo la picha la simba sc 2017

Mchezo huo utaanza Saa 8:00 mchana na baadae utafuatiwa mchezo wa pili wa kundi hilo kati ya Jang’ombe Boys ya Zanzibar na Gor Mahia ya Kenya hapo hapo Uhuru.

Michuano hiyo ilianza jana Uwanja wa Uhuru, mabingwa wa Tanzania wakiwang’oa mabingwa wa Kenya, Tusker FC kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 4-2 baada ya sare ya 0-0 ndani ya dakika 90.

Yanga yatinga nusu fainali ya SportPesa Super Cup Kibabe!!

Jana vigogo wa Kenya, AFC Leopards nao waliitupa nje Singida United kwa penati 5-4 kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 pia.

Bingwa wa michuano hii atajinyakulia kitita cha dola za Kimarekani 30,000 zaidi ya Tsh 60 na atapata nafasi ya kucheza mchezo wa kirafiki na Klabu ya Everton kutoka England mwezi ujao.

By Godfrey Mgallah 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents