Burudani

Quick Rocka atia neno mvutano wa Barakah The Prince na Ben Pol

Msanii wa Bongo Fleva, Quick Rocka amesema wimbo mpya wa Ben Pol ‘Tatu’ aliomshirikisha Darassa kwa upande wake anaona ni mzuri kwani amekuja na kitu kipya chenye ubunifu.

Quick Rocka

Wiki iliyopita msanii Barakah The Prince kupitia kipindi cha XXL cha Clouds FM alimkosoa Ben vikali kwa kudai wimbo huo ni mbaya kulingana na tension aliyoitengeneza mwanzo.

Baraka The Prince

Quick Rocka amekiambia kipindi cha E Newz cha EATV, kauli ya Barakah The Prince ni kama mtazamo tu wa kila mtu huwezi kumzuia mtu kuongea kama kitu ni kibaya kwanini aseme anapenda wakati hajakipenda.

Ben Pol

“Huo ni mtazamo wake mimi naona wimbo ni mzuri, amekuja na idea tofauti. Darassa kachana vizuri, beat Tiddy Hotter kapiga vizuri, it nice song kwangu mimi. Sasa ungemtafuta Barakah akuambie yeye ameona ubaya gani,” amesema Quick.

Msanii huyo ameongeza kuwa kinachotokea kwa Ben Pol sasa hivi maana yake anakua zaidi, changamoto zinapozidi kwenye maisha maana yake unapanda step halafu mambo yanakuwa mazuri.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents