Burudani

Juma Nature amekosa kampani yangu ndio maana ‘anafeli’ – Fella

Mkurugenzi wa Yamoto Band na TMK Wanaume Family, Mkubwa Fella amedai Juma Nature anashindwa kufanya vizuri kwenye muziki kutokana na kukosa huduma yake.

Meneja huyo amedai yeye alikuwa anajua njia za kupita kumpromote muimbaji huyo na kuhakikisha kazi zake zinafika kwa wananchi.

“Juma Nature muziki wake haujapungukiwa chochote, yule kapungukiwa kampani yangu. Kwa sababu alichokuwa anafanya ni kile kile, ila kwa sasa amekosa kampani yangu,” alisema Mkubwa Fella. “Mimi naweza kuongea na mwenye redio vizuri, mimi naweza kuongeza na Dj vizuri. Juma Nature anaimba vizuri pia ni mtunzi mzuri kwahiyo mimi nachoweza kusema kwa Nature ni hilo,”

Fella alisema yupo tayari kufanya tena kazi na Juma Nature lakini Nature ameonekana kutokuwa tayari kufanya tena kazi na meneja wake huyo wa zamani.

Nyimbo nyingi za Juma Nature za hivi karibuni zimeshindwa kufanya vizuri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents