Burudani

Video: Dayna Nyange aeleza kwanini habanduki kwa Mr T Touch

Msanii wa Bongo Flava, Dayna Nyange ameeleza sababu ya kupenda kurekodi ngoma zake kwa producer Mr T Touch.

“Huwa sipendi kuhama, najikutana nafanya kazi sehemu moja ikitokea nikafanya kazi nyingine nafanya. Najikuta napenda kufanya naye kazi kwa sababu ni mtu ambaye anafanya kazi vizuri ameshakaa na mimi na ameshajua Dayna uwezo wake ni upi,” Dayna ameiambia Bongo5.

“Wimbo wangu wa sasa Chovya umefanywa na maprodyuza wawili ambao ni Mr T Touch na Moko Genius ambaye nilishaenda kwenye studio yake kufanya kolabo kama mbili akaniambia natamani tufanye kitu, hivyo akatengeneza beat pale tukafanya kazi lakini ilimaliziwa kwa Mr T Touch, na ni watu ambao wanaelewana,” ameongeza.

Dayna Nyange kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Chovyo’ ikiwa ni ngoma ya tatu kufanya kwa Mr T Touch baada ya kutoa hit kama Angejua na Komela.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents