Habari

Video: DC Jokate amsaidia mama wa watoto mapacha waliyoungana maini kupata nyumba ya kisasa na bima ya Afya

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Mh, Jokate Mwegelo amemsaidia mama aliyejifungua watoto mapacha waliyo ungana maini kupata bima ya afya na nyumba bora ya kuishi kutoka UBA United Bank for Africa hii inakuja mara baada ya mama huyo pamoja na watoto wake kupata ruksa ya kurejea nyumbani kwao Kisarawe.

Mama huyo wa watoto mapacha Gracious na Precious Michael Mkono wamepata ruksa rasmi katika Hospitali ya Muhimbili mara baada ya kufika hapo toka tarehe 21/07/2018 kupata matibabu baada ya kujifungulia nyumbani.

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imefanikiwa kufanya upasuaji huo wa kuwatenganisha mapacha hao walioungana wakiwa chini ya miaka mitatu, ambao wamezaliwa Kisarawe mkoani Pwani, Julai 12, mwaka huu. Jumatano ya Septemba 26, Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Profesa Laurence  Moselu, alisema upasuaji huo uliofanyika Septemba 23, kwa mafanikio makubwa ilienda vizuri.

Kwa mujibu wa Daktari bingwa wa upasuaji kwa watoto Dkt. Petronila Ngiloi amesema mapacha hao walizaliwa na mama yao aitwaye Esta (22) nyumbani kwao Kisarawe, alikozalishwa nyumbani baada ya kugundua watoto wameungana walipelekwa Kituo cha Afya cha Kibaha na baadaye kuhamishiwa Muhimbili wakiwa wamechoka sana.

Amesema watoto hao walipochunguzwa iligundulika wameungana sehemu kubwa ya ini na ikaonekana upasuaji huo unaweza kufanyika MNH ambapo walifanya kazi ili kuona mama huyo anapata huduma nzuri

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents