BurudaniDiamond Platnumz

Video: Diamond, Mohombi, Davido na Lumino washoot video ya remix ya Rockonolo Gabon, itafanyika Bongo pia

Rockonolo, wimbo ambao Diamond, Mohombi na Lumino waliutumbuiza Jumamosi kwenye ufunguzi wa kombe la mataifa ya Afrika, AFCON 2017, nchini Gabon, unaweza kuwa moja ya nyimbo kubwa za Afrika mwaka huu.

Lumino na Diamond

Wimbo huo ni wa Lumino na amewashirikisha mastaa hao kwenye remix yake.

Lumino, Mohombi na Diamond

Jumapili hii, mastaa hao wameshoot video yake na kumwalika staa wa Nigeria, Davido kuungana nao.

Haijaishia hapo tu, Diamond amedai kuwa Jumanne hii pia watashoot vipande vingine vya video hii jijini Dar.

“Leo tulifanikiwa kushoot video ya #Rockonolo Remix GABON… tutashoot pia vipande kadhaa nchini Tanzania siku ya Jumanne, je ungependa kuwa mmoja wapo?” ameandika kwenye Instagram.

Mohombi akiwa na Davido

Hajaeleza iwapo Mohombi na Lumino nao watakuja Dar kwaajili ya kushoot vipande hivyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents