Michezo

Video: Fataki za Ubalozi wa Marekani Dar zawarusha roho wananchi

Wakazi wa maeneo ya Morroco na Msasani jijini Dar es Salaam usiku wa Alhamis walijikuta wakiingiwa na hofu kubwa baada ya kusikia milio inayofanana na risasi iliyokuwa ikisikika kutoka kwenye ubalozi wa Marekani. Wananchi wengi walihisi ni tukio la uvamizi katika eneo la Msasani City Mall. Hata hivyo, sauti hizi zilikuwa za fataki zilizokuwa zikipigwa ubalozi hapo muda ambao timu ya Marekani ilikuwa ikicheza na Ujerumani kwenye kombe la dunia ambapo Marekani imeingia hatua ya mtoano licha ya kufungwa na hivyo kuwafanya wengi waamini kuwa fataki hizo zilikuwa ni ishara ya kushangilia kwa hatua hiyo.

Haijafahamika mara moja iwapo ni kweli fataki hizo zilipigwa kwa sababu ya Marekani kusonga mbele kwenye michuano hiyo. Hizi baadhi ya video zilizowekwa kwenye Instagram zinazoonesha tukio hilo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents