Burudani

Video: Hii ndiyo ndinga ya Fid Q aina ya Jeep

Msanii wa muziki wa hip hop, Fareed Kubanda aka Fid Q ameamua kuonyesha gari lake jipya aina ya Jeep Renegade Lift Kit yenye rangi ya ‘Bluu bahari’ kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram.

Kupitia mtandao huo Fid Q, ameandika ujumbe unaosomeka ‘ChengaChengaZaKekiYangu’ huku akionyesha gari hilo.

”Weekend njema waungwana, #ChengaChengaZaKekiYangu,” ameandika msanii huyo wa muziki wa hip hop, Fareed Kubanda aka Fid Q.

Siku za hivi karibuni Msanii huyo aliingia kwenye kutoelewana na baadhi ya viongozi wa WCB, hali iliyopelekea mmoja wa viongozi hao kuandika ujumbe kuwa hana gari.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents