Michezo

Video: Luis Suarez amng’ata mlinzi wa Italia,Chiellini

Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez amekumbwa na kashfa mpya baada ya kumng’ata mlinzi wa Italia, Giorgio Chiellini katika mchezo wao wa jana wa kombe la dunia ambapo Uruguay iliibuka kwa ushindi wa bao moja bila.

Suarez-main

Suarez alionekana akiminya bega la Chiellini muda mchache kabla ya Diego Godin kufunga bao la ushindi la Uruguay dhidi ya Italia.

http://youtu.be/8W8VC-WY-V8
Chiellini aliangushwa chini na uchungu wa meno ya Suarez na alionekana akimkimbilia refari akimvulia shati ilikuonesha alama ya meno begani lakini refarii akapuzilia mbali. Chiellini ameiambia runinga moja ya Italia kuwa Suarez alijiangusha chini likuficha uovu huo wa kutisha na kusingizia kuwa alikuwa amepigwa kumbo.

Pia Suarez aliwahi kukaa nje mechi 10 baada ya kumng’ata kiungo wa Chelsea, Branislav Ivanovic April 2013.

Chiellini-bite

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents