Habari

Video: Mabaki ya mwili wa binadamu yapatikana Vatican

Mabaki ya mwili wa binadamu yamepatikana katika ubalozi wa Vatican nchini Italia huku vyombo mbalimbali vya habari vikiyahusisha na binti wa kike mwenye umri wa miaka 15 ambaye amewahi kupotea mwaka 1983.

A military soldier guards the entrance of the Apostolic Nunciature, the Vatican's embassy to Italy, in Rome, Wednesday, Oct. 31, 2018. The Vatican said Tuesday that human bones were found during renovation work near its embassy to Italy, reviving talk about one of the Holy See's most enduring mysteries - the fate of the 15-year-old daughter of a Vatican employee who disappeared in 1983.  (Fabio Frustaci/ANSA via AP)

Taarifa kutoka Vatican inasema kuwa polisi wanajitahidi kubaini umri na jinsia ya mwili wa mifupa hiyo, na siku ambayo kifo kilitokea.

Vyombo vya habari vya Italia vimesema kuwa mabaki hayo huenda ni ya msichana wa miaka 15 wa mfanyakazi wa Vatican aliyepotea mwaka 1983

Reporters film the entrance of the Vatican embassy to Italy, Tuesday, Oct. 30, 2018. The Vatican said Tuesday that human bones were found during renovation work near the embassy, reviving speculation once again about one of the most enduring Vatican mysteries: the fate of Emanuela Orlandi, the 15-year-old daughter of a Vatican employee who disappeared in 1983. (AP Photo/Alessandra Tarantino)

Kwa mujibu wa shirika la habari la ABC, Hii leo siku ya Jumatano wanasheria wa familia ya binti huyo aliyepotea mwaka 1983 akiwa na umri wa miaka 15 wamewasisitiza waendesha mashitaka na Vatican kutoa habari zakina kuhusiana na mabaki hayo ya mifupa yaliyopatikana kwenye ubalozi huo huko Rome.

Habari hizo za kuonekana kwa mabaki hayo ya mifupa ya mwanadamu zilitangazwa jana siku ya Jumanne na kuamsha hisia za uwezekano wa kuwa mwili huo ukawa ni wa Emanuela Orlandi mtoto wa mfanyakazi wa Vatican.

FILE - In this May 27, 2012, file photo, demonstrators hold pictures of Emanuela Orlandi reading "march for truth and justice for Emanuela" during Pope Benedict XVI's Regina Coeli prayer in St. Peter's square, at the Vatican. The Vatican says human bones were found during renovation work near its embassy to Italy, reviving speculation once again about the fate of Orlandi, the 15-year-old daughter of a Vatican employee who disappeared in 1983. (AP Photo/Andrew Medichini, File)

Shirika la habari la ANSA limeripoti kuwa waendesha mashitaka walikuwa wakifatilia kama mabaki hayo yanaweza kuwa ni binti huyo Orlandi, ambaye alipotea Juni 22 mwaka 1983, au msichana mwingine mwenye umri wa miaka 15, Mirella Gregori, ambaye alipotea Mei 7, 1983 huko Roma.

“Tunawauliza waendesha mashitaka wa Roma kama mabaki hayo yatakuwa na mahusiano yoyote na msichana aliyepotea Emanuela Orlandi na Mirella Gregori,” mwanasheria Laura Scro amesema.

Taarifa kutoka Vatican inasema kuwa polisi wanajitahidi kubaini umri na jinsia ya mwili wa mifupa hiyo, na siku ambayo kifo kilitokea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents