Burudani

Video: Mfahamu Beka the Boy kutoka nchini Kenya

Beka the Boy ni miongoni mwa wasanii wachache ambao wamekuwa wakiangaziawa na vyombo vya habari nchini Kenya kwa jinsi anavyojituma kwenye kazi yake ya muziki.

Beka the Boy anatokea katika Pwani ya Kenya na kwa muda wa miaka mitatu kwa sasa amekua akiburudisha Wakenya kwa ngoma kama kama vile Niko Low, Jidai, Siri ya Moyo, Msanii, Tena bado, Utanikumbuka, Najuta, Nimefall na sasa ana tamba na kibao kipya kwa jina la Nyota.

Alianza muziki wake mwaka wa 2013 akiwa muimbaji wa band ya Sea Waves iliyoko mjini Malindi kwa kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kuanza kufanya kazi solo artist ambapo aliweza kufanya kazi na Malindi Records.

Hata hivyo kwa sasa staa huyu wa muziki anatamba na video yake mpya ‘Nyota’ iliyoongozwa na waongoziji wa muziki wawili wakubwa Africa na raia wa Kenya Dr. Eddy wa Dreamland Entertainment wanaohusika kuongoza video za wasanii wakubwa kama Jose Chameleon, King Kaka, Octopizzo na wengineo.

Stori na Changez Ndzai, Kenya

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents