Burudani

Video: Mshindi wa Super Nyota afunguka kuhusu wimbo wake, ugumu alioupata kwa Dully Sykes

Mshindi wa mwaka jana wa mashindano ya Super Nyota, Nchama The Best ambaye ameachia ngoma yake mpya ‘Tufanye Kesho’ aliyomshirikisha Dully Sykes amefunguka kuhusu wimbo huo.

Rapper huyo ameiambia Bongo5, kuwa wimbo huo ni kwaajili ya watu wenye roho mbaya ambao hawapendi kuona mwenzao akifanikiwa. “Kuna vitu ume plan kuvifanya, halafu mtu anatokea tu hujui ametokea wapi anataka kuja kukukatisha, kukuwekea vikwazo kwamba usiendelee kuvifanya vile vitu, kwa hityo unamwambia kwa leo sipo vizuri hebu tufanye kesho,” amesema msanii huyo.

Nchama ameendelea kwa kusema, alitumia muda kama wa wiki moja mpaka kumpata mkongwe Dully na kumweka katika wimbo huo.

Msanii huyo ameongeza kuwa anamipango ya kwenda kushoot video japo hata moja nje ya nchi ingawa Tanzania bado kuna location nyingi nzuri hazijatumika. “ Ukiangalia Tanzania ni nchi ambayo inasifika sana kwa kuwa na mandhari nzuri. Wakati nipo mtaani huko nilikuwa napambana kuwakilisha mtaa wangu, Mungu akanisaidia nikafanikiwa. Nilivyofanikiwa nikataka tena niitangaze tena Mwanza katika nchi yangu ya Tanzania pia nimefaulu kwa hilo, kwa hiyo sasa hivi nina focus kuitangaza nchi yangu kimataifa zaidi,” amesema.

“Kuna Uganda ambapo natamani siku moja kushoot video. Kuna mandhari nzuri sana, siwezi nikaelezea lakini ni nchi nzuri sana.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents