Habari

Video: Mwanachama ambaye safari imemshinda ashuke mwenyewe – Mh. Zitto

Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe amesema chama hicho kinaheshimu maamuzi ya mtu yoyote hivyo mwanachama ambaye anaona safari imemshinda ya kuendelea na chama hicho ashuke mwenyewe.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Zitto amesema wanachama wanaodhani kama chama hicho ni jukwaa la kuisifia Serikali wajitathimini au kuchukua hatua.

“Tulimwita Mwigamba katika kikao cha chama aje kutueleza kama tunakikuka misingi ya chama kama alivyosema lakini hakufika. Chama kinaheshimu mchango wa kila Mwana-ACT, lakini tunawashauri wanaondoka wasiwashawishi wanachama wengine kuondoka au kusema mambo ya uongo dhidi ya Chama kwani kufanya hivyo ni sawa na kunyonga mtoto uliezaa mwenyewe, mwanachama ambae safari imemshinda ashuke mwenyewe ,”

Hata hivyo Zitto pamoja na hayo amesema kuwa chama hicho kina ahadi tano ni (1)kupambana na dhuluma, fitina, unafiki, uongo, rushwa na ufisadi kwa uwezo wangu wote (2)Nitapigani kuwepo kwa demokrasia ndani na nje ya Chama Changu na nyinginezo.

Viongozi waliokihama chama hicho ni Samson Mwigamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Kampeni wa ACT – Wazalendo na wenzie 10, Prof. Kitila Mkumbo ambaye kwasasa ni Katibu Mkuu wizara ya Maji.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents