Michezo

Antonio Conte aogopa kivuli chake

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte amesema atakuwa mchawi endapo atatabiri timu yake kufikia mafanikio kama yaliyopatikana msimu uliyopita katika kipindi hiki cha kutetea ubingwa wao wa EPL.

Conte raia wa Italia ameiongoza Chelsea kunyakuwa taji la ligi kuu nchini Uingereza kwa mara yake ya kwanza akikiongoza kikosi hiko cha Stamford Bridge msimu uliyopita na hatimae amegundua kuwepo na ugumu wa kutetea taji hilo msimu huu.

Chelsea ambayo itashuka dimbani hii leo kuwakabili Watford inashika nafasi ya tano huku ikizidiwa pointi tisa juu ya vinara wa ligi, klabu ya Manchester City.

The Blues imekuwa na matokeo ya kutoridhisha hivi karibuni dhidi ya City, Crystal Palace na kutoka sare ya mabao 3-3 siku ya Jumatano mbele ya Roma katika michuano ya klabu bingwa barani Ulaya.

Hatahivyo Conte hajakata tamaa na matokeo anayoyapata huku kusisitiza kukabiliana nayo hadi atakapo yapatia ufumbuzi na wala haogopi kukabiliana na nyakati ngumu.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents