Habari

Video: Nimekuwa mpole sana – Mhe. Nape

Mbunge wa Jimbo la Mtama, Mhe. Nape Nnauye amesema kuwa watu wanaoanza kumchambua yeye kuanzia kwenye Uwaziri wanakuwa wamekosea yeye ameanza kuongea akiwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa 2002, hivyo anaemjua tangu kipindi hicho kwasasa atakuwa anamshangaa kwasababu amekuwa mpole sana.

Mhe. Nape ameyazungumza hayo katika mahojiano yake na Bongo5 aliyoyafanya hivi karibuni mjini Dodoma ambapo amesema alikuwa ni mtu anaeongea anacho kiamini.

“Kuna watu wanaanza kumchambua Nape kuanzia kwenye Uwaziri ukianzia hapo utakosea, mchambue Nape mimi nimeingia kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya taifa 2002 kwa mara ya kwanza miaka 15 sasa ndio nimeingia kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu, nadhani nilikuwa ni mjumbe wa Mahakama Kuu niliyekuwa vocal katika watu ambao nilikuwa na speak my mind naongea ninacho kiamini actually, nilianzi pale kwahiyo kwa mtu anaenijua ananishangaa leo nimekuwa mpole sana nimekuwa sisemi sana wakati huo nilikuwa nasema sana,” alisema Nape.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents