AFCON 2019 Tupogo!
Vodacom Data Datani!

Video: Rapper Meek Mill alivyokaribishwa kifalme kwenye NBA

Meek Mill amefanikiwa kupata mapokezi ya kifalme kwenye timu yake ya nyumbani kwao Philadelphia ya mchezo wa kikapu, Sixers ambayo amekuwa akiishabikia kwa muda mrefu.

Rapper huyo alihudhuria kwenye mchezo wa ligi kuu ya mpira wa kikapu Marekani (NBA) jana kwenye uwanja wa Wells Fargo Center ikiwa ni muda mfupi mara baada ya kutoka gerezani kwa dhamana kuishuhudia timu yake hiyo iliyokuwa imeshuka dimbani kucheza na Miami Heat.

Katika mchezo huo wa tano Sixers ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya vikapu 104 dhidi ya 91 vya Miami Heat.

Mpaka sasa Sixers wameshinda jumla ya michezo minne wakati Miami ikiwa imeshinda mchezo mmoja pekee.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW