Habari

Video: Serikali yaja na utaratibu huu kuhusu kupanga ada elekezi kwa shule binafsi

Serikali itaamua ada elekezi kwa shule binafsi nchini kwa kuzipanga shule katika makundi maalum kulingana na huduma na ubora wa shule hizo.

Feza Schools

Akijibu swali bungeni Jumatano hii lililoulizwa na mbunge wa Kawe, Halima Mdee kuhusu kauli ya serikali kuhusu kubaini gharama ya kumsomesha kila mwanafunzi wa shule ya bweni na kutwa kwa shule binafsi, Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi,Teknolojia,Ufundi na Mafunzo ya Ufundi,Eng. Stella Manyanya, alisema hatua hiyo imekuja baada ya serikali kufanya utafiti.

Alidai kupitia utafiti huo, walibaini kuwa gharama katika shule hizo zinatofautiana kwa kiasi kikubwa kulingana na huduma zinazotolewa, aina ya shule na miundombinu iliyopo.

Amesema serikali ilifanya mazungumzo taasisi mbalimbali zinazohusika na shule hizo ili kupanga ada elekezi kwa pamoja.

“Wizara sasa imeanza zoezi la kupanga shule hizi kwa makundi ili kuweka viwango vya ada kwa kuzingatia ubora na huduma ili kutoathiri kiwango cha elimu inayotolewa,” alisema.

Eng Manyanya aliongeza kuwa utaratibu huo hautaathiri kiwango cha elimu kinachotolewa kwenye shule binafsi.

Alitolea mfano kuwa kupitia utafiti huo walibaini kuwa kuna shule binafsi zilizopo vijijini kwenye maeneo ya mikoani zinazotoza ada ya shilingi laki moja huku shule ya sekondari ya Feza ya Dar es Salaam ikitoza ada ya shilingi milioni 9.4, St Joseph shilingi milioni 5.9 na Mwanza Alliance shilingi milioni 4.8.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents