Michezo

Video: Stars ilivyoilaza Lesotho katika kuwania nafasi ya tatu ya COSAFA

Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imefanikiwa kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Cosafa baada ya hapo jana kuifunga Lesotho kwa mikwaju ya penalti 4-3.

https://youtu.be/OAR1ihNTRUc

Stars imeibuka na ushindi huh baada ya kutoshana nguvu ndani ya dakika 90 za bila kufungana na kuruhusu kupigwa kwa mikwaju ya Penati. Katika michuano hiyo inayoendelea nchini Afrika Kusini, Mchezaji Shiza Ramadhani Kichuya ndiye aliyekuwa wa kwanza kupiga na kukosa Penati.

Hata hivyo baadaye wachezaji wa timu ya taifa ya Lesotho walipoteza penati mbili, moja ikigonga mwamba na nyingine ikiokolewa na golikipa Said Mohamed ‘Nduda’ na kuiwezesha Tanzania kuibuka katika nafasi ya tatu ya michuano hiyo mikubwa akiwa kama mgeni mwalikwa.

Wafungaji wa penati kwa upande wa Tanzania ni Himid Mao, Simon Msuva, Abdi Banda na Raphael Alpha aliyema malizia kazi na Shiza Kichuya a;iyekosa penati ya kwanza.

Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents