Michezo

Video: Tukiacha rushwa na figisu tutayafikia mafinikio ya Everton – Dk. Mwakyembe

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dr. Harrison Mwakyembe amezitaka klabu za Tanzania kuacha rushwa na figisu figisu ili kufikia mafanikio ya klabu ya Everton ya nchini Uingereza.

Dk Mwakyembe, alisema kuwa ujio wa klabu hiyo utawafanya vijana wa Tanzania kupata fursa ya kuiga na kujifunza mengi kutoka kwa timu hiyo inayoshika nafasi ya 7 katika msimu 2016/17 wa ligi kuu ya Uingereza.

Klabu ya Everton Julai 13 mwaka huu itacheza na mshindi wa michuano ya SportPesa Super Cup.

Jumla ya timu 8 zitashiriki michuano hiyo na kwa upande wa Tanzania ni pamoja na klabu ya Young Africa Sport, Simba SC, Singida United bila kusahau timu kutoka Zanzibar na kwa upande wa nchini Kenya timu zitakazo shiriki ni Nakuru All Stars, AFC Leorpads , Gor Mahia pamoja na klabu ya Tusker FC.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents