Burudani

Video: Vibaka wampora ripota akiwa live kwenye TV, SABC

Mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha SABC, Vuyo Mvuko aliporwa na vibaka wakati akiwa live kwenye TV nje ya hospitali ya Milpark huko Parktown, Johannesburg jana jioni,

Mvuko alikuwa akiripoti kuhusu ziara ya rais wa Edgar Lungu aliyekuwa kwenye hospitali hiyo kutibiwa Malaria.

Video hiyo inamuonesha Mvuko na mtu wake wa kamera akizingirwa na vijana watatu ambao mwanzoni wanaonekana kama wapita njia lakini walisimama mbele na nyuma ya ripota huyo wakitaka wapewe simu na fedha.

Vibaka hao walichukua vitu kadhaa vya Mvuko huku pia wakimfuata camera woman aliyekuwa hapo. Mwishoni mwa video hiyo, Mvuko anasikika akisema: We are being mugged.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents