BurudaniVideos

Video: Waganda Wapagawisha

Moze Radio and Weasle

 

Wasanii wawili wanaounda kundi la GoodLyfe Moze Radio na Weasle kutoka jijini Kampala nchini Uganda Iumaa ya wikiendi iliyopita waliweza kupagawisha mashabiki wa muziki wao waliohudhuria katika shoo ya Boogie FurahiDay.

Shoo hiyo ambayo inakwenda kwa jina la Boogie Furahiday ambayo hufanyika kila ijumaa ya mwisho wa mwezi ilifanyika katika klabu ya usiku ya New Maisha iliyopo masaki jijini Dar Es-Salaam ambapo wasanii hao waliimba zaidi ya nyimbo saba na kupagawisha mashabiki ambao waliimba nao tangu kuanza kwa shoo hadi mwisho.

Nyimbo kama Nakudata, Bread and bata, Vuvuzela, Zuena na nyinginezo kali zililipua mayoe katika klabu ambapo wakina dada wengi walionekana kupagawa zaidi wakiimba na kucheza huku wengine wakitaka kupanda stejini.

Bongo5 ilikuwepo ukumbini na hapa chini ni vipande vya video vya shoo hiyo.

{hwdvs-player}id=1236|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1235|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

{hwdvs-player}id=1234|tpl=playeronly{/hwdvs-player}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents