Habari

Video: Wanawake wawili wauawa kikatili, watatu washikiliwa na polisi

Wanawake wawili ambao ni mtu na shangazi yake, Kija Lushanga mwenye umri wa miaka 70 na Pendo mwenye umri wa miaka 40 ambaye jina la baba yake halikuweza kufahamika mara moja wamekutwa wamefariki huku viungo mbalimbali vya miili yao ikiwemo kichwa, viganja vya mikono, sehemu za siri, na matiti vikiwa vimeondolewa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jeshi la polisi lilifika katika eneo la tukio na kukuta kiganja kimoja kikiwa kimesahaulika na hadi sasa linawashikilia watu watatu wanaosadikiwa kuhusika na mauaji hayo.

Tukio hilo limetokea majira ya saa tano asubuhi ya leo katika Kijiji cha Lubanga Tarafa ya Kasamwa Wilayani Geita baada ya wanawake hao wanaosadikiwa kuvamiwa na watu wasiojulikana kushambuliwa kwa mapanga.

Chanzo Azam tv.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents