Michezo

Video ya mchezaji wa NFL akimpiga ngumi mkewe kwenye lifti hadi kuanguka na kuzimia yasambaa

Rais Barack Obama wa Marekani amemlaani vikali mchezaji wa timu ya football Baltimore Ravens, Ray Rice baada ya video inayoonesha akimpiga ngumi mchumbawa wak, Janay Palmer hadi kuanguka chini akizimia wakati wakibishana wakiwa kwenye lifti.

Tukio hilo lilitokea huko Atlantic City mwezi February mwaka huu lakini video hiyo imewekwa na mtandao wa TMZ jana Jumatatu. ‘Rais ni baba wa watoto wawili wa kike. Na kama Mmarekani yeyote yule, anaamini ukatili majumbani haukubaliki katika jamii iliyostaarabika,” yalisema maelezo kutoka ikulu ya Marekani.

Janay ni mke wa Rice kwa sasa.

“Kumpiga mwanamke si kitu mwanaume halisi hufanya na hiyo ni kweli haijalishi ukatili huo unatokea kwenye macho ya umma ama kama ilivyo mara nyingi ndani.”

Kutokana na kuonekana kwa video hiyo, chama cha mpira huo nchini Marekani, NFL (National Football League) kimemsimamisha mchezaji huyo. Rice alikuwa akicheza kwa mkataba wa miaka mitano kwa dola milioni 40 tangu July 2012.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents