Wabunge wahoji baada ya Rostam kutoswa

Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wamehoji sababu za Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Aziz, kutopewa fursa ya kujieleza kuhusiana na tuhuma zinazomkabili kwa mujibu wa Kamati Teule ya Bunge

Rostam Aziz


 


Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wamehoji sababu za Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Aziz, kutopewa fursa ya kujieleza kuhusiana na tuhuma zinazomkabili kwa mujibu wa Kamati Teule ya Bunge iliyochunguza tuhuma za kampuni ya Richmond.



.
Wakizungumza mjini hapa jana kwa masharti ya kutotajwa majina, wabunge hao walisema ni haki ya mbunge huyo kujieleza hasa kutokana na kutuhumiwa kuwa alisingizia kuwa nje ya nchi na kushindwa kufika kutoa ushahidi mbele ya Kamati hiyo.


 


Mmoja wa wabunge hao alisema huenda Bw. Rostam amejiandaa ‘kupasua mabomu’ ambayo yanaweza kusababisha mkanganyiko ndani na nje ya Bunge, na hivyo inachukuliwa tahadhari na ndiyo sababu ya kucheleweshwa kupewa nafasi.


 


“Unajua mtu huyu anaweza kuwa na mambo mazito ya kuwasilisha bungeni, naamini anajua vitu vingi na kwa kuwa ameshajeruhiwa, anaweza kupasua chochote kikaleta mtafaruku … pengine Spika anajiweka sawa kwa hilo, akimhofia,” alisema.


 


Habari kutoka ofisi ya Spika, zilisema Bw. Rostam alifika ofisini hapo juzi mchana kueleza nia ya kutaka kuwasilisha maelezo yake bungeni, lakini Spika akamkatalia kuwa hataweza kufanya hivyo mpaka awe amewasilisha maelezo hayo kwa maandishi.


 


Alitakiwa kufanya hivyo siku moja kabla ya kusimama bungeni kuwasilisha maelezo hayo, habari jana zilisema juzi jioni aliwasilisha maelezo hayo na kusubiri pengine jana angepewa nafasi hiyo.


 


Pamoja na kutojitokeza kutoa ushahidi mbele ya Kamati hiyo iliyokuwa chini ya Mbunge wa Kyela, Dkt. Harrison Mwakyembe, Mbunge huyo wa Igunga anatuhumiwa pia kudai kuwa Kamati hiyo ilifanya kazi nje ya muda wake uliopangwa.


 


Alipozungumza na gazeti hili, Bw. Rostam alisema yeye yuko tayari na amezingatia kanuni zote ikiwa ni pamoja na kuwasilisha maelezo yake kwa Spika kwa maandishi.


 


 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents