Michezo

Wachezaji wa Ujerumani wawapigia magoti mashabiki wao ‘tulistahili kutolewa’

Baada ya kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Dunia, wachezaji wa timu ya taifa ya Ujerumani wamewaomba radhi mashabiki wao kwa kichapo cha goli 2-0 dhidi ya Korea Kusini.

Kupitia ukurasa rasmi wa Twitter wa mabingwa hao watetezi wa Kombe la Dunia, wamesema kuwa kwenye mchezo huo hawakucheza kama mabingwa na ndio maana wametolewa kwenye hatua ya makundi.

Mashabiki wetu wapendwa! hata sisi tumeumizwa kama nyinyi, Kombe la Dunia linachezwa kila baada ya miaka minne na tumekuwa tukijitahidi sana kwa muda wote. Tunaomba radhi, hatujacheza kama mabingwa wa Dunia, kwa hiyo tulistahili kutolewa kama matokeo yalivyokuwa ingawaje yanaumiza.

Ujerumani imetolewa kwa mara ya kwanza kwenye hatua ya makundi tangu kombe la dunia la mwaka 1938 lililofanyika nchini Ufaransa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents