Habari

Wafahamu mafundi seremala wanao tengeneza majeneza aina ya gari, ndege na pilipili

Mafundi seremala nchini Ghana wameamua kufika mabali zaidi katika utengenezaji wa majeneza kwa kuongeza ubunifu wao ili kuendana na soko pamoja na mahitaji ya wateja zao.

65835

Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, watengenezaji hao wanajivunia zaidi kutengeneza majeneza yanayoashiria maisha, ndoto na hadhi ya marehemu, wapendwa wa marehemu wanaamini kuwa anastahili kuagwa kwa heshima kubwa kwa hivyo mazishi yake sharti yazingatie mambo yote muhimu yanayoangazia maisha yake.

65788

Wanahabari Fellipe Abreu na Henrique Hedler walitembelea karakana mbili za Kane Kwei, katika Mji Mkuu wa Accra na Kumasi, kukutana na maseremala marufu wanaounda majeneza.

Coffin

Maduka hayo yamepewa jina la Seth Kane Kwei, ambaye baadhi ya wenyeji wanasema ni mtu wa kwanza kuunda jeneza la aina yake nchini Ghana.

Ghana ni moja mataifa yanayokuza zao la cocoa kwa wingi duniani, kwa hivo familia hasa zinazoishi katika maeneo ya vijijini hutumia pesa wanazopata kutokana na zao hilo kuwafanyia wapendwa wao mazidhi ya kifahari kwa kuwaundia majeneza ya kipekee.

65051

Jeneza kama hili linaweza kugharimu hadi dola 1,000 (sawa na euro 780) – hiki ni kiwango kikubwa sana cha pesa kwa wakulima, ambao wengi wao wanajimudu kupata chini ya dola 3 kwa siku.

Kwa mfano katika picha hii “pilipili inaashiria mengi zaidi ya maisha ya mkulima”, anasema msimamizi wa karakana Eric Adjetey, ambaye amekuwa katika biashara hii kwa miaka 50.

65771

Ndege pia ni moja ya miundo maarufu ya majeneza, hili ni la mtoto

Rangi nyekundu na mapambo mengine yaliyotumiwa yanaangazia tabia ya marehemu. “Alikuwa mkali na mwenye hasira za haraka, huyu ni mtu huwezi kudhubutu kumchezea.”

Majeneza yenye muundo wa gari aina ya Mercedes Benz ni maarufu sana – Jeneza hili ni la mtu tajiri ambaye alikuwa anamiliki gari holo na kaburi lake litachimbwa jinsi litakavyotoshea.

“Hili ni moja ya majeneza yanayotumika sana, yanaashiria hadhi ya mtu katika jamii,”anasema Steve Ansah muundaji wa majeneza.

Watu wengi wanayaita majeneza haya vipande vya sanaa ya kifahari, lakini wenyeji wanayaita Abeduu Adekai, kumaanisha “masanduku ya methali”.

65794

Wakati mwingine jamii huchangisha pesa za kugharamia majeneza haya.

Katika miaka ya hivi karibuni uwekezaji katika sekta ya nyumba umeongezeka sana nchini.

Jeneza hili ni la mmilili wa nyumba za kupangisha ambaye alienziwa sana na jamii yake kwa kuwajengea nyumba za makaazi.

65756

“Mara nyingu huwa ni jukumu la familia ya marehemu kununua jeneza, Lakini pia wananasimamia hafla ya maisha ya mpendwa wao kwa kununua chakula,maji na vinywaji.”

Bwana Adjetey anasema “Sherehe hiyo hufanyika kuanzia Alhamisi hadi Jumatatu.

Siku ya Alhamisi famila inaleta jeneza; Siku ya Ijumaa mwili unatolewa katika chumba cha kuhifadhi maiti.

Siku ya Jumamosi mazishi inafanyika, na siku ya Jumapli watu wanaenda kanisani. Jumatatu familia inahesabu pesa zilizotumika na zile zilizochangishwa na wahisani.

Maseremala hutengeneza jeneza kisha wanayalainisha kwa kutumia kifaa maalum kabla ya kupaka rangi.

65704

Kuna msanii wa muziki atakayezikwa kwa jeneza hili lenye muundo wa kipaza sauti.

”Huwa hatujui kimo cha marehemo kwa hivyo tunauliza familia yake na mara nyingine tunatumia hata picha ya marehemu” Anasema Ansah mmoja wa waundaji majeneza haya.

Katika miaka ya hivi karibuni, maseremala wengine pia wameanza kutengeneza majeneza haya ya kipekee kutokana na ongezeko la watu wanayoyahitaji.

Uundaji wa majeneza ya aina hii umewavutia wanafunzi wanaosomea useremala nchini Korea Kusini, Urusi, Marekani na Denmark, ambao wanazuru Ghana kujifunza sanaa hiyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents