Habari

Wafungwa miaka 30 kwa unyang’anyi

WAKAZI watatu wa kijiji cha Sirari wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na kuchapwa viboko 12 baada ya kupatikana na kosa la kumng’oa meno sita mfanyabiashara wa mjini Tarime John Rotente na kumpora simu na f

Makubo Haruni, Tarime

 
WAKAZI watatu wa kijiji cha Sirari wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela na kuchapwa viboko 12 baada ya kupatikana na kosa la kumng’oa meno sita mfanyabiashara wa mjini Tarime John Rotente na kumpora simu na fedha.

 

 

 

Waliohukumiwa kutumikia adhabu hiyo na Hakimu Mkuu Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Tarime, Alivunge Mallya, wametajwa kuwa ni Raphael Masero, Nyamanga Range na Sokoine Range ambao walikuwa wakikabiliwa na kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha Februari 2, mwaka huu.

 

 

 

Kabla ya Hakimu Mallya hajasoma hukumu hiyo, Mwendesha Mashitaka wa Polisi, Kija Mkoi alidai watu hao kwa pamoja walimvamia mfanyabiashara huyo huko Sirari wakiwa na mapanga na kumkatakata mkono wa kushoto, wakampiga kichwani kwa rungu na kusababisha meno sita kung’oka.

 

 

 

Mkoi alidai licha ya kumjeruhi mlalamikaji huyo, pia watu hao watatu walimpora simu ya Nokia yenye thamani ya Sh 200,000 na Sh milioni 1.2.

 

 

 

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mallya alisema kwa kuwa wahalifu ni vijana ambao wangefanya kazi ya halali badala yake wakachukua uamuzi wa kufanya vitendo vya uhalifu kwa kumng’oa meno Rotente na kumharibia mfumo wa mdomo sambamba na kumpora fedha. Licha ya kufungwa, pia Hakimu huyo aliwaamuru kumfidia mlalamikaji.

 

 

 

Wakati huo huo, mkazi wa kijiji cha Nyantira, Bhoke Kimwama (20) juzi alikufa baada ya kuchomwa kisu wakati akinywa gongo takriban mita 100 kutoka kituo kidogo cha polisi kijijini hapo.

 

 

 

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Nonosius Komba amesema kuwa tukio hilo lilitokea juzi wakati wa ugomvi uliomhusisha marehemu. Mtuhumiwa wa mauaji hayo amekamatwa na atafikishwa mahakamani muda wowote uchunguzi utakapokamilika.

 

 

 

Source: Habari Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents