MichezoUncategorized

Wagombea TFF  kampeni ruksa hadi kesho asubuhi – Kuuli

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wakili Revocatus Kuuli amewaambia wagombea kuwa, wapo huru kufanya kampeni zao hadi asubuhi ya kesho Jumamosi kabla ya upigaji kura kuanza.

Kuuli amesema kampeni hizo wameruhusu zifungwe kabla ya shughuli ya uchaguzi kuanza saa 2:00 asubuhi.

Hapo awali Kamati ya Uchaguzi ilitangaza muda wa siku tano wa kufanya kampeni hizo ambapo zilipaswa kufungwa leo Ijumaa saa sita usiku.

“Kila kitu kinakwenda sawa kabisa, tumeruhusu kampeni zifanyike hadi kesho asubuhi kabla ya kuanza uchaguzi, kampeni hizo ni zile za chini chini na utulivu mkubwa ili zisiingiliane na ratiba nyingine.

“Tutakapoanza taratibu zingine kama kuhakiki hapo ndio zitafungwa rasmi, kikubwa narudia kuwaomba wagombea na wapiga kura kuzingatia umakini kwani sheria zipo wazi,” amesema Kuuli.

Jumla ya w agombea 65 wapo mjini hapa tangu Jumatano wakitengeneza mazingira kwa wapiga kura huku kila mgombea akionekana anapambana kivyake kuomba kura na ulinzi wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) ukiwa umeimarisha kila kona jambo ambalo linawapa hofu wagombea kufanya mambo tofauti na kanuni, taratibu na sheria za nchi.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents