Habari

Waliotaka kuzitafuna fedha za tetemeko Kagera wapandishwa kizimbani

Viongozi watatu wa serikali na meneja wa benki ya CRDB, wamefikishwa mahakamani ya Bukoba kwa tuhuma za kula njama kwa kufungua akaunti za bandia inayofanana na ile ya maafa ya waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera

chademaa-1

Watumishi hao wamepandishwa kizimbani Alhamisi hii mkoani humo huku wakikabiliwwa na mashtaka mawili ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kufungua akaunti feki ya maafa Kagera yenye kesi namba 239/2016.

Waliopandishwa mahakamani ni pamoja na aliyekuwa ofisi tawala mkoa wa Kagera (RAS) Amantius Msole na aliyekuwa mkurugenzi wa manispaa ya Bukoba, Kelvin Makonda, aliyekuwa mhasibu mkoani Kagera Simbaufoo Swai na meneja wa benki ya CRDB Kagera, Carlo Sendwa.

Wakili wa serikali Hashimu Ngole, alisema watuhumiwa hao wanashtakiwa na makosa mawili, kushirikiana kufungua akaunti feki linalofanana na akaunti ya maafa ya Kagera,na lingine ni kutumia vyeo na madaraka yao kinyume na sheria.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents