Burudani

Wanachoiga Harmonize na Sarah kutoka kwa Zari na Diamond

Moja ya couple tulivu ambayo haina drama nyingi kwa sasa Bongo ni ile ya Harmonize na mpenzi wake Sarah, wamekuwa pamoja kwa kipindi kirefu sasa tangu pale Harmonize alipoachana na aliyekuwa mpenzi wake Wolper.

Kutokana na utulivu katika mahusiano yao waandishi wa habari za kidaku ni mara chache sana kutupia jicho kujua kile kinachoendelea kati yao ukilinganisha na couple za mastaa wengine ambao waandishi kila uchwao hupata hile na hile kutokana na drama zao.

Sarah ni binti mdogo kutoka nchini Italy ambaye anatajwa kumiliki mkwanja mrefu kwa kiasi chake. Hilo halimzuii kuongozana na muimbaji huyo wa WCB katika show ambazo huenda kuzifanya sehemu mbali mbali.

December 31, 2017 Harmonize alifanya show kubwa sana Mtwara akishirikiana na wasanii kama Shilole, Queen Darleen, Lava Lava Young Killer, Stereo na wengineo. Katika show hiyo Harmonize aliongozana na Sarah mkoani humo kuanzia promotion ya show hadi siku ya tukio lenyewe.

Sarah na Harmonize wakiwa Rwanda

Kwa sasa wawili hao wapo nchini Rwanda ambapo Harmonize anataraja kufanya show hapo kesho. Utakumbuka ni takribani miezi mitatu imepita baada ya kuonekena pamoja katika show nyingine.

Kabla ya Diamond na Zari kuachana mara kadhaa walikuwa wakiongozana katika show ambazo alikuwa akifanya muimbaji huyo.

Zari na Diamond wakielekea Naivasha, Kenya kwa ajili ya show

October mwaka jana Diamond alikuwa na show visiwani Zanzibar na waliongozani. Hii ilikuwa ni baada ya kuwepo taarifa kuwa wameachana zikiwa ni wiki kadhaa kupita tangu Diamond kukiri kuwa alizaa na mwanamitindo Hamisa Mobetto.

Baada ya hapo waliongoza hadi Naivasha nchini Kenya ambapo Diamond pia alikuwa na show. Hiyo ni mifano tu ya miezi ya hivi karibuni lakini huko nyuma wamefanya hivyo mara kadhaa.

Harmonize na Sarah nao bila shaka kuna vitu viwili vitatu walivipata kutoka kwenye mahusiano ya Diamond na Zari hasa katika upande huo niliyouelezea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents