Habari

Wanaume Halisi wafanya kufuru!!

Juma NatureHayawi hayawi!! hatimaye yakawa!…hii ilikuwa ni kwenye uzinduzi wa kufa mtu kuwahi kutokea ktk miaka ya karibuni ambapo kundi la ‘Wanaume Halisi’..lilikuwa likizindua albam yao ya kwanza.

Hayawi hayawi!! hatimaye yakawa!…hii ilikuwa ni kwenye uzinduzi wa kufa mtu kuwahi kutokea ktk miaka ya karibuni ambapo kundi la ‘Wanaume Halisi’..lilikuwa likizindua albam yao ya kwanza.


Ilikuwa sio rahisi kuamini lakini ukweli ni kwamba idadi ya mashabiki walihudhuria uzinduzi huo ilikuwa ya kutisha na kwa hesabu za haraka haraka pamoja na uzoefu wangu wa kuhudhuria kwenye matamasha kadhaa ya Bongo Flava….naweza kusema uzinduzi huu umeweza kabisa kuvunja rekodi ya maonyesho mengine likiwamo lile la ‘Ugali’ la msanii Juma Nature.


Kundi hilo lililojitenga kutoka katika kundi la ‘Wanaume TMK’, lilitumbukia Diamond Jubilee likiwa limetinga mavazi ya Kichina, huku baadhi yao baadhi yao wakiwa wamenyoa vipara na kuanza kucheza katika mtindo wa ‘Makung Fu Complex’.


Huku wakiwa wanashangiliwa na mashabiki wengi waliokuwa ukumbini hapo, Wanaume Halisi waliokuwa wanaongozwa na Juma Nature na Inspekta Haroun walianza kuimba nyimbo zikiwamo zile za zamani kama ‘Mzee wa Busara’, ‘Mtoto wa Geti Kali’ kabla ya mwisho kumaliza na ‘Ndege Tunduni’ ambao ulikuwa unasubiriwa na mashabiki wengi.


Wasanii wengine walionogesha zaidi uzinduzi huo ni pamoja na Jose Chameleon kutoka Uganda ambaye alikonga mashabiki na nyimbo zake ‘Jamila’, ‘Kipepeo’ na ‘Ndivyo Sivyo’ alioshirikiana na Profesa Jay.


Nonini na kundi la P Unit kutoka Kenya pia walifanya vizuri na nyimbo za ‘Keroro’ na ‘Si Lazima’, huku wasanii kutoka hapa nyumbani kama Fid Q, Mabaga Fresh, Chid Benzino, Joh Makini, Afande Sele wakikonga nyoyo za mashabiki ukumbini hapo.


BOFYA HAPA KUONA PICHA ZA SHOW

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents