Michezo

Wanawake wajitokeza kwa wingi kuwania uongozi wa chama cha soka (TWFA)

Chama cha Mpira wa Miguu wanawake (TWFA),kimetangaza rasmi wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi ujao untakaofanyika Julai 8 mwaka huu,kuwa ni Amina Karuma (Nafasi ya Uenyekiti); Rose Kissiwa (Makamu Mwenyekiti); Somoe Ng’itu (Katibu) na Theresia Mung’ong’o (Katibu Msaidizi).

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Msomi Wakili George Mushumba ameongoza kikao cha Kamati ya Uchaguzi na kupitia majina ya wagombea walioomba kugombea nafasi mbalimbali.

Nafasi ya Mweka Hazina, kwa mujibu wa Mushumba inawaniwa na Hilda Masanche ilihali nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu TFF, inawaniwa na Salma Wajesso na Zena Chande huku Ujumbe wa Kamati ya Utendaji TWFA waliopitishwa ni Triphonia Temba, Jasmine Badar, Chichi Mwidege na Mwamvita Kiyogomo.

Musumba ametangaza majina hayo ya wagombea waliostahili au waliotimiza taratibu za uchaguzi kwa mujibu wa katiba na kanuni za uchaguzi za TWFA.

Kinachofuata kwa sasa ni kwamba Juni 26 na 27, 2017- Kupokea pingamizi kati ya saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika ofisi za TFF.

Juni 28, 2017- Kamati ya Uchaguzi kupitia pingamizi kama zimewasilishwa.

Juni 29, 2017- Kamati kutoa majumuisho ya pingamizi kama ziliwasilishwa na wadau.

Juni 30, 2017- Usaili kwa wagombea waliotangazwa.

Julai 01, 2017- Kutangaza majina ya wagombea waliopitishwa

Julai 02, 2017-Kamati kupokea rufaa

Julai 03, 2017- Kamati kupitia rufaa kama zimewasilishwa.

Julai 04, 2017 Kamati kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea.

Julai 04 hadi 07, 2017 – Wagombea kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili.

Julai 08, 2017- Uchaguzi Mkuu wa TWFA

.……………………………………………………………………………………………..
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents