Michezo

Warriors wachukua ubingwa wa NBA baada ya kuwasambaratisha Cavs (Video)

Vijana wa Steve Kerr Golden State Warriors wamekuwa mabingwa wa ligi ya mpira wa kikapu nchini Marekani kwa mara ya pili mfululizo katika ushindi wa vikapu 108 dhidi ya vikapu 85 huku Kevin Durant kutoka Warriors akishinda tuzo ya MVP (Most Valuable Player) kwa msimu wa pili mfululizo lakini pia Warriors wanashinda fainali yao ya tatu kati ya fainali nne walizokutana na Cleveland Cavalies huku Cavs akishinda fainali moja tu mwaka 2016 kuanzia mwaka 2015,2017 na 2018 ndo misimu ambayo Warriors walikuwa mabingwa ingawa kwa miaka yote ikiwa imetwaa taji hilo kwa nyakati 6 tofauti tofauti.
https://youtu.be/SUdL8JXn0pI

Kwahiyo kwa mara ya pili mfululizo Kombe hilo linaelekea Zone ya Werstern ambapo fainali ilianza mey 31 katika uwanja wa Warriors unaojulikana kama Oracle Arena,Okland Carfonia michezo miwili na yote Warriors wameshinda michezo mingine miwili ikafanyika Ohio uwanja wa nyumbani wa Cavs vile vile michezo yote Warriors wameshinda na kuwa na jumla ya michezo minne walioshinda kati ya michezo saba ambayo wangetakiwa kucheza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents