Habari

Wasanii 400 kushiriki Sauti za Busara Zanzibar

Sautiza BusaraZAIDI ya wasanii 400 maarufu na chipukizi watashiriki kwenye tamasha la Nne Sauti za Busara litakaloanza kuunguruma kuanzia Februari hadi 14, mwaka huu

Sauti za BusaraMwandishi wa Habari Leo

 

ZAIDI ya wasanii 400 maarufu na chipukizi watashiriki kwenye tamasha la Nne Sauti za Busara litakaloanza kuunguruma kuanzia Februari hadi 14, mwaka huu katika eneo Ngome Kongwe visiwani Zanzibar.

 

Tamasha hilo la siku sita lililojipatia umaarufu mkubwa Afrika na hata Ulaya, litazinduliwa kwa onyesho filamu ya Bi Kidude ya “As Old As My Tongue: The Myth & Life of Kidude” inayohusu maisha ya msanii huyo mkongwe iliyotengenezwa Zanzibar na Ulaya miaka minne iliyopita.

 

Kwa mujibu wa waandaaji, tamasha hilo litatanguliwa na warsha ya siku tatu kwa wasanii na zaidi kwa wale ambao wanatoka nchi ambazo hutumia lugha ya Kiswahili kwa ajili ya kujenga na kubadilishana mawazo kisanii na ujuzi mbalimbali.

 

“Na mwaka huu pia kutakuwa na kitu kipya na muhimu kwa washiriki kwani kutakuwapo semina ya wazi ya bure kwa washiriki watakaopenda kujifunza masuala ya menejimenti ya muziki pamoja na mbinu za kutafuta masoko,” alisema Mkurugenzi wa Sauti za Busara, Yusuf Mahmoud jana alipozungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam.

 

Tamasha la mwaka huu litakuwa na mambo mengine mapya ikiwamo kusherehekea ufunguzi wa tamasha kwa kuandamana kupitia mitaa ya Stone Town siku ya ufunguzi. Pia kutakuwapo
sherehe za kufunga tamasha Siku ya Wapendanao kwenye Hoteli ya Kendwa Beach.

 

Baadhi ya wasanii watakaokuwapo kwenye tamasha la mwaka huu ni Jose Chameleone, Fid Q, MB Dogg, Matonya, Juma Nature na Wanaume Halisi wakiwa na Inspekta Haroun, Luteni Kalama, Dolly, Rich One, na Nako2Nako.

 

Source: Habari Leo

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents