Promotion

Washindi wa ‘Shinda na M-Pawa’ kutoka Vodacom wafunguka ‘hatukuamini, tulijua tunatapeliwa’ (+video)

Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom kushirikiana na Benki ya CBA wiki hii wamewakabidhi washindi watatno wa Bajaj na mshindi mmoja milioni 10 kupitia promosheni yao ya Shinda na M-Pawa.


Washindi watano wa bajaji wakiwa wamefurahia sana ushindi huo wameisifia benki ya CBA na Vodacom kwa mkakati wao wa kuirejeshea jamii fadhila kwa njia ya kuwezesha wananchi huku wakiwataka wateja wa M-Pawa kuendelea kutumia M-Pawa na kuwakaribisha ambao bado hawajaanza kutumia kujiunga.

Washindi hao wakizungumzia zawadi hizo, wengi wameoneshwa kufurahishwa huku wakielezea kuwa wakati walivyopigiwa simu kupewa taarifa hawakuwa wanaamini.

Mshindi wa milioni kumi ni Mama Sophia Sarapion (54) ni mwenyeji wa Bukoba ambapo anaishi akijushughulisha na shughuli ya kilimo cha mihogo, Benki imepanga kumtembelea mshindi huyo mwezi ujao. Washindi watano wa bajaji ambao ni AbeidAbeid, Lucas Ngoye, MariamuBarawa, Hassan MsabilanaHamisiMpela wanatokea maeneo tofauti tofauti ya Tanzania ambayo ni Arusha (1),Chalinze (1) Dar Es Salaam (3).

Mama Sophia ambaye amefurahi sana ameishukuru benki ya CBA na Vodacom kwa kuunda promosheni hii akisema “M-Pawa haijanisaidia tu kwenye maisha yangu ya kila siku linapokuja swala la kutunza akiba na kupata mikopo inayoniwezesha kufanikisha mipango yangu bali imebadilisha maisha yangu kabisa.Nitatumia fedha hizi vizuri  katika kuboresha shughuli yangu ya kilimo”

Washindi watano wa bajaji wakiwa wamefurahia sana ushindi huo wameisifia benki ya CBA na Vodacom kwa mkakati wao wa kuirejeshea jamii fadhila kwa njia ya kuwezesha wananchi huku wakiwataka wateja wa M-Pawa kuendelea kutumia M-Pawa na kuwakaribisha ambao bado hawajaanza kutumia kujiunga.

Akizungumza kwenye sherehe hiyo ya makabidhiano ya zawadi hizi kwa washindi, Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa benki ya CBA Bwana Julius Konyani alieleza “Promosheni ya SHINDA NA M-PAWA ililenga kuwafikia wananchi wasiofikiwa na huduma za kibenki na kuwawekea mazingira ya kujiwekea akiba huku ikiwapa changamoto ya kurudisha mikopo yao kwa wakati pale wanapokuwa wamechukua mkopo.Mikopo yetu ina riba ndogo sana kwani lengo letu hasa ni kuwawezesha kiuchumi wateja wetu.Lengo letu jingine ilikuwa kuwashukuru na kuwazawaida wateja wetu msimu huu wa sikukuu.Tunafurahi washindi wetu wameweza kuwa ishara ya mafanikio yetu katika lengo hili.

Benki ya CBA kwa ushirikiano na Vodacom tutaendelea kutoa huduma hii ya Mpawa kuweza kuwafikia watanzania wengi zaidi, wakiwemo wakulima na wajasiriamali kuweza kuwakwamua kwa kuwapa mikopo midogo midogo ya mpaka shilingi laki tano. Mbali na hayo M-Pawa inawapa fursa wateja kuhifadhi hela zao kwa malengo yao ya baadae, akiba yako ndio Malengo yako. Katika kipindi hichi cha promosheni tumefanikiwa kuwapata wateja wapya zaidi ya milioni moja wa M-pawa, hivyo Mpawa imekuwa na jumla ya watumiaji wa huduma hii wanayokaribia milioni nane.

Nawapongeza sana washindi wetu wote zaidi ya 1200 na pongezi za kipekee kwa mshindi mkuu na washindi watano waliojishindia bajaji wakawe mabalozi wetu popote watakapopita na waendelee kuhamasisha matumizi ya Mpawa.”

Kampeni ya SHINDA NA M-PAWA ilifanyika kwa muda wa wiki 6 kuanzia tarehe 8 Novemba hadi tarehe 13 Desemba ikilenga watumiaji wa huduma ya M-Pawa.Jumla ya washindi 1,296 walipatikana katika kipindi hicho cha promosheni.Huu ni Ushahidi kwamba jitihada za benki ya CBA na Vodacom katika kuwafikia wananchi wasiofikiwa na huduma za kibenki zinaendelea vyema.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents