Tupo Nawe

Watanzania wa chini waendelea kuondoka na magari ya kisasa kupitia promosheni ya Faidika na Jero

YUSUPH Jacksoni Murimi(29), Mkazi wa Serengeti jana alikabidhiwa rasmi gari yake aina ya Renault Kwid mara baada ya kuibuka mshindi kwenye promosheni ya Faidikana Jero.

Promosheni ya Faidika na Jero ilidumu kwa siku 40 ambapo watumiaji wa mtandao wa Tigo kupitia huduma ya TigoPesa walipata nafasi ya kujishindia zawadi mbalimbali ikiwemo smartphone kila siku na siku ya mwisho zawadi ya gari.

Akizungumza wakati wa makabidhiano, Yusuph alisema kuwa “Ukirudia mazungumzo yangu siku ya kwanza wakati napigiwa simu utagundua kwamba nilikuwa siwaamini walionipigia simu kama ni kweli SportPesa maana siku hizi mjini watu hawatabiriki.

“Nilikuwa nacheza tu lakini sikutarajia bahati hii ya ushindi wa gari itanidondokea mimi.

 

“SportPesa wamenipa mapokezi mazuri ikiwemo kusimamia gharama zote kuanzia usafiri wa ndege, malazi pamoja na matumizi ya siku nzima na kuhakikisha gari langu linapata usajiri kupitia jina langu na kukabidhiwa”

“Sijui nisemeje lakini nawashukuru sana SportPesa, mimi nimuajiriwa kwenye kampuni kama fundi welder nasikutarajia kama siku ningeweza kushinda zawadi ya gari” “Nawasihi vijana wenzangu wacheze na SportPesa maana kwa sasa nawaona hawana mpinzani, nasio kama unapoteza pesa. Mimi nilikuwa nacheza na kushinda kwa kubashiri mechi kama sehemu ya burudani lakini leo nimejionea dhahiri kuwa kuna zaidi ya ushindi”

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW