Burudani ya Michezo Live

Watu bilioni 3.2 wanatumia internet duniani

Namba ya watu duniani wanaotumia internet ilifikia bilioni 3.2 hadi mwishoni mwa mwaka 2015, lakini waliosalia, bilioni 4.1 bado hawajafikiwa na huduma hiyo kwa mujibu wa utafiti uliodhaminiwa na Facebook.

Internet

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka wa pili ya Facebook, ‘State of Connectivity’ imeonesha kuwa watu wapya milioni 200 walifikiwa na internet mwaka 2015 kutokana na kupungua kwa gharama za huduma hiyo.

Ripoti hiyo imedai kuwa nchi zinazoendelea bado zimeachwa nyuma.

‘Urban areas are connected, many rural areas are not. The less money you have, the less likely you are to be online. In many countries, women use the Internet far less than men. And even if the entire world lived within range of the necessary infrastructure, nearly a billion people remain illiterate or otherwise unable to benefit from online content,’ imesema ripoti hiyo.

Imedai kuwa kama hakutakuwa na mabadiliko ya kuirahisisha huduma hiyo, hadi mwaka 2020 watu bilioni 3 wataendelea kutofikiwa na huduma hiyo, wote wakiwa katika nchi zinazoendelea.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW