Habari

Nape Nnauye: Wakati nikisoma nilifikiria kuwa rubani wa ndege tena ndege za kijeshi

Waziri wa habari,utamaduni,wasanii na michezo Nape Nnauye amesema kuwa wakati anakuwa ndoto yake kubwa ilikuwa ni kuwa rubani wa ndege za kivita.

Nape+PHOTO

Akiongea kwenye 255 XXL ya Clouds FM, Nape alisema ndoto hizo ndizo zilimfanya asome sana masomo ya Fizikia, Jiografia, na Hesabu(PGM) ila kwa bahati mbaya akafeli fizikia jambo lililomfanya kuhamia kwenye uchumi (EGM).

“Mwanzo kabisa wakati nikisoma nilifikiria kuwa rubani wa ndege tena ndege za kijeshi sikutaka ndege za kawaida na ndio maana kwenye elimu yangu ya sekondari nilisoma sana masomo ya sayansi.”

“Kwa bahati mbaya sikufanya vizuri somo moja kwahiyo nikashindwa kuendelea na hayo masomo nikaamua kusoma uchumi EGM, kama ni kazi niliyotamani kufanya ni kuwa rubani wa ndege lakini baadaye nikapoteza hamu ya kufanya lakini nafikiri mbele ya safari kama wataniruhusu kurusha ndege za kawaida,” alifunguka Nape.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents