Habari

Watu zaidi ya 250 wafariki katika maporomoko nchini Colombia

Watu takribani 254 wamedaiwa kufariki dunia katika maporomoko ya ardhi yaliyotokea katika mji wa Mocoa nchini Colombia baada ya mvua kubwa iliyonyesha Jumamosi.

Vikosi vya uokoaji vinavyoendesha shughuli hiyo vimesema kikwazo kikubwa kwenye zoezi hilo ni barabara nyingi za huko eneo la mji wa kusini mwa mji huo hazipitiki kutokana na kuharibiwa na maporomoko hayo.

Hata hivyo imedaiwa kuwa kuna uwezekano mkubwa wa idadi hiyo kuongezeka kutokana na watu wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 200 hawajaonekana mpaka sasa.

Rais Juan Manuel Santosa wa nchi hiyo alitangaza hali ya tahadhari katika eneo hilo na kusafiri kuangalia shughuli za uokoaji zinavyoendelea.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents