Watuhumiwa Epa kizimbani

Hatimaye mafisadi wanaotuhumiwa kuchota mabilioni ya fedha kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), jana walifikishwa mahakamani na kufunguliwa mashitaka ya kughushi na kujipatia mamilioni ya fedha toka Benki Kuu ya Tanzania

Watuhumiwa Epa  kizimbani

 

HATIMAYE mafisadi wanaotuhumiwa kuchota mabilioni ya fedha kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), jana walifikishwa mahakamani na kufunguliwa mashitaka ya kughushi na kujipatia mamilioni ya fedha toka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Jumla ya watu 10, akiwemo mfanyabiashara maarufu Jayantkumar Chandubhai Patel, maarufu kwa jina la Jeetu Patel, pamoja na wafanyakazi wa BoT walifikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Washitakiwa hao walipandishwa kizimbani kwa nyakati tofauti huku mshitakiwa namba moja katika kesi hiyo, Johnson Lukaza akipandishwa peke yake kujibu tuhuma za kula njama na kughushi na kuiibia BoT zaidi ya Sh6.3 bilioni.

 

Watuhumiwa Epa  kizimbani

 

 

Mbele ya Hakimu, Euphemia Mingi, wakili wa serikali Winie Koroso alidai kuwa, kati ya Desemba 2003 na 2005 mshitakiwa alighushi hati ya kuhamishia mali toka kampuni ya Kernel na Maruben ya nchini Japan ambayo ilikuwa inaonyesha imetolewa Februari 4 mwaka 2005.

Hata hivyo, mshitakiwa huyo alikana shtaka hilo na Hakimu Mingi aliahirisha kesi hiyo mpaka Novemba 18 itakapotoa maamuzi ya dhamana.

Katika kesi nyingine washitakiwa watatu akiwemo Jeetu Patel na ndugu zake wawili Devendra Patel na Amit Nandy walipandishwa kizimbani kujibu tuhuma za kula njama na kuiibia BoT zaidi ya Sh 2.5 bilioni.

Washitakiwa hao, ambao walifikishwa mbele ya Hakimu Neema Chusi, kwa pamoja wanadaiwa kuwa kati ya Agosti 7 na Desemba 7 mwaka 2005 jijini Dar es Salaam walikula njama za kuiibia BoT Sh2,599,944,456.12 na kuziwakilisha katika kampuni ya Matsushita Electric Trading.

Katika kesi hiyo mshitakiwa wa tatu Amit Nandi anadaiwa kughushi hati iliyoonyesha kuwa kampuni hiyo ya Matsushita inaidai BoT kiasi hicho cha fedha.

Wakili Koroso aliendelea kudai kuwa Septemba 2 mwaka 2005 washitakiwa walikula njama ya kuiibia BoT Sh3.9 bilioni baada ya kusaini mkataba kati ya kampuni ya Bina na C. Itoh za nchini Japan.

Washitakiwa hao walikana mashtaka yao na mahakama imeahirisha kesi hiyo hadi leo itakapotoa maamuzi ya dhamana yao.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents