Michezo

Wazazi wa Alphonce Simbu wanena mazito (Video)

Baba mzazi wa mwanariadha Alphonce Simbu, Mzee Felix Simbu amesema anafuraha kubwa kuona mwanae amefanya vizuri katika mashindano makubwa na kuiletea sifa Taifa.

Wazazi wa mwanariadha, Alphonce Simbu,(Mzee Felix Simbu na Bi Salome Tandu Mvua) wakiwa Uwanja wandege kwaajili ya mapokezi ya mtoto wao

Simbu ambaye ni baba mzazi wa Alphonce Felix Simbu ameyasema hayo wakati akizungumza na Bongo5.

“Ninafuraha kubwa pamoja na watanzania wezangukuona kijana amefanya vizuri, kwakweli ameanza kujifunza kukimbia tangu yupo shule ya Msingi mkoani Arusha”, amesema baba wa mwanariadha Simbu.

Mzee huyo ameongeza kuwa “Nilikuwa nikifurahi kumuona Simbu akiwa anashiriki masomo na michezo hivyo natoa ushauri kwa wazazi wenzangu kutokuwazuia watoto waige mfano wake”.

“Nilivyokuwa shuleni nimekuwa nikishiriki michezo mingi hasa ya kukimbia na magunia, riadha na kucheza mpira ilikuwa ndiyo kazi yangu ingekuwa kipindi kama hiki ningekuwa mbali na mabao mengi walikuwa wakiyapata kwaajili yangu nikiwa namba 11 uwanjani”.

Wakati mama mzazi wa mwanariadha huyo, Bi Salome Tandu Mvua akizungumzia namna alivyomlea kijana huyo “Haina ya malezi niliyomlea yalikuwa mazuri na hakuwahi kunisumbua hata alivyokuwa anasoma”.

“Ushindi aliyoupata wa kushika nafasi ya tatu katika michuano ya riadha ya dunia naubariki tu”, amesema Bi Tandu Mvua.

By Hamza Fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents