Habari

Waziri Kigwangalla atoa sadaka kwakunusurika kwenye ajali ‘Matokeo ya ajali ile yangeweza kuwa mabaya zaidi’

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla ameamua kutoa sadaka ikiwa ni kama njia ya kumshukuru Mungu kwa kuokoa maisha yake baada ya kufikwa na ajali mbaya ya gari aliyoipata Agosti 4 mwaka huu huko mkoani Manyara.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamis Kigwangalla

Dkt Kigwangalla ameyasema hayo mbele ya kadamnasi ya watu ambapo sadaka hiyo atakayoitoa akisema kuwa ni kuwasomesha watoto watano bure huku akisisitiza kuwa amekuwa na desturi ya kusomesha watano na sasa uakiongeza na hao wengine watakuwa jumla idadi yake wanafikia 10.

”Matokeo ya ajali ile yangeweza kuwa mabaya zaidi kuliko haya niliyoyapata, kwahivyo kwa lolote lililonitokea sina laziada bali kumshukuru Mungu kwa neema zake.” amesema Dkt Kigwangalla

Dkt. Hamis Kigwangalla  ameongeza ”Nimeamua katika kuchukua hatua hiyo ya kumshukuru Mungu ni kutoa sadaka ya kusomesha watoto watano zaidi, kila mwaka huwa nasomesha watoto watano bure kwenyechuo ambacho kinaendeshwa na mkewangu pale Nzega Mjini.”

”Nimeamua kuongeza watano wengine iliiyende ikawe sadaka yangu kwa hivyo nitafanya utaratibu wakuweza kupata majina hayo watoto wengine watano zaidi ambao nitawasomesha pale kwenye chuo cha mkewangu na nitaendelea kuwasomesha watoto 10 kila mwaka katika chuo kile bila ya kutoa tozo yoyote ile.”

https://www.instagram.com/p/BpcEjDvh76k/?taken-by=azamtvtz

Kwenye ajali hiyo iliyotokea mapema asubuhi ya Agosti 4, imeweza kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye alikuwa ni afisa habari.

Marehemu Hamza Temba enzi za uhai wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents