Waziri mkuu aliombe Bunge Radhi-Lipumba

Waziri Mkuu wa jamuhuri ya muungano wa tanzania Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda ametakiwa kuliomba radhi Bunge la Jamhuri ya Muungano na Watanzania kwa ujumla,

lipumba_1.jpg

 

Waziri Mkuu wa jamuhuri ya muungano wa tanzania Mheshimiwa Mizengo Kayanza Pinda ametakiwa kuliomba radhi Bunge la Jamhuri ya Muungano na Watanzania kwa ujumla, kutokana na kauli yake Bungeni juu ya msimamo wa Serikali kuhusu kampuni tata ya Meremeta.

Shinikizo hilo kwa Waziri Mkuu limetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof. Ibrahim Lipumba, baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa vyombo vya dola nchini tayari vimeshalichunguza suala hilo na kubaini kuwepo kwa wizi wa fedha za Watanzania, na kuwa hivi sasa vinajiandaa kuwaburuza wahusika mahakamani. Prof.

Lipumba amesema leo kuwa Waziri Mkuu anapaswa kuelewa kila kinachofanywa na Serikali na kuwa alistahili kuwaeleza wabunge ukweli kuwa suala hilo linafanyiwa kazi na vyombo vya dola, hivyo analazimika kuomba radhi kutokana na makosa hayo aliyofanya.

“Waziri Mkuu anapaswa kuliomba radhi Bunge kwa kutolipatia taarifa sahihi, maana lilikuwa jambo la kuwaeleza wabunge tu kuwa suala hilo linafanyiwa kazi na vyombo vya dola, lakini hakufanya hivyo” akasema Prof.

Lipumba. Prof. Lipumba amedai kuwa hivi sasa inaonyesha kuwa kuna matatizo ya mawasiliano ndani ya Serikali, kiasi kwamba kila mmoja anazungumza lake na kujikuta wakitofautiana katika suala moja. Akitoa mfano wa kujikanganya, Prof.

Lipumba amesema, Waziri wa Fedha, Bw. Mstafa Mkullo hivi karibuni alilieleza Bunge kuwa fedha zilizochotwa katika akaunti ya Madeni ya Nje, EPA, sio za Serikali, lakini Waziri Mkuu akasema lazima fedha hizo zirejeshwe serikalini.

Wiki iliyopita wabunge walihoji uhalali wa kampuni ya Meremeta na kumtaka Waziri Mkuu atoe ufafanuzi, ambapo Mbunge wa Kigoma Kaskazini alifikia hatua ya kusema kuwa mradi huo ulikuwa ni wizi wa fedha za Watanzania.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents