Habari

Waziri mkuu awataka wataalam wa ujenzi wa makazi ya Magomeni kota kujenga kwa wakati

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka watalaamu wa ujenzi wa mradi wa nyumba za makazi Magomeni watumie utaalamu wao vizuri na wakamilishe kwa wakati.

kot1-768x465

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na wajenzi wakati alipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Nyumba, Magomeni Kota jijini Dar es salaam kukagua mendeleo ya mradi huo Novemba 18, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri mkuu ametoa agizo hilo wakati akikagua ujenzi wa nyumba hizo zinazojengwa na wataalam kutoka Wakala wa Majengo Tanzania(TBA) eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam.

“Tunahitaji sasa tuprove tuna uwezo wa kujenga haya maghorofa mawili kwa miaka mingi wahandisi wetu mmefanya vizuri,majengo mengi mmejenga nyie na sasa ni taasisi yetu TBA kuprove kwamba inaweza kufanya kazi hii vizuri, na majengo mnayojenga nyumba za serikali za kawaida kwasababu mnaingia kwenye teknolojia nyingi ya ujenzi wa nyumba za majengo ya kwenda juu,”alisema Majaliwa.

“Muhimu mjue kwamba mmepewa dhamana hii kubwa ya kukamilisha ujenzi huu ili wananchi waliokuwa wanaishi hapa waweze kurudi katika makazi yao,” aliongeza.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents