BurudaniDiamond PlatnumzUncategorized

WCB ni chama la wana – Diamond

Msanii wa Bongo Flava na Mmiliki wa Label ya WCB, Diamond Platnumz amesema label hiyo ni kwa ajili ya msanii yeyote yule, hivyo ni mapema kusitisha zoezi la kuchukua wasanii wengine hasa wale wanaochipukia.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Eneka’, ameiambia  XXL ya Clouds Fm kuwa WCB itaendelea kuchukua wasanii wapya ila itatengemea zaidi support watakayozidi kupata kutoka kwenye vyombo vya habari.

“Unajua sisi tunasemaga WCB ni chama la wana kwa sababu sisi tunajaribu kuchukua watu wa aina tofauti tofauti kutoka kwenye mtaa na mimi siwezi kuwasaidia pekee yangu ndio maana namleta kwenye media ili afikie malengo yake na watu wengi wapo mitaani wanaohitaji msaada,” amesema Diamond na kuongeza.

“Kwa hiyo tukisema tunaaacha ina maana unakatisha ndoto za vijana wengi ambao wanaamini wanaweza kuwa ndani ya WCB, lakini support tutakayopata ndio itasema tuendelee kusainisha watu au tusitishe, kama support hamna  mimi mwenyewe Diamond Platinumz nitaachia mangoma yangu,” amesisitiza.

WCB hadi sasa ina wasanii sita ambao Harmonize, Rich Mavoko, Queen Darleen, Rayvanny, Lava Lava na Diamond mwenyewe.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents